Muda ni Sasa by Natasha Shyrose


                                                                 Song: Muda ni Sasa
Artist: Natasha Shyrose ft Jimmy Luv Producer: WaterflyMusic  Cover design: Magne Hoven

Lyrics:
Bora kosa kila kitu duniani lakini si muda
ukipata shukuru ukikose haurudi
Huwezi fanikiwa bila changamoto
Maisha ni mtihani kuna kufeli na kupasi
uwezo wako utakuonyesha marafiki na wanafiki
Wajali wanaokujali wape muda wako
Na kama kila mtu anakupenda huna kitu unachowazidi
mmmmmmm

Rusha mikono angani
Tuliza kifuani
Sikiliza
Mapigo ya moyo wako
Mapigo

Chorus.
Muda ni sasa
muda ni sasa
muda ni sasa

Kama hujawahi vunjika moyo
Hujawahi kupenda
Mapenzi ni ahadi
Mara nyingi huvunjwa
Na kama hujawahi kusalitiwa
Hujawahi amini
Binadamu ni dhaifu
Kutunza wake utu
Hakuna anayepigwa vita kama msema ukweli
Anaharibia wengi uongo wanaouamini
ishi kwa furaha jinsi vile nafsi yako inavyopenda
Uwe huru

Rusha mikono angani
Tuliza kifuani
Sikiliza
Mapigo ya moyo wako
Mapigo

Chorus.
Muda ni sasa
muda ni sasa
muda ni sasa

Rap:
NÃO IMPORTA O QUE ACONTEÇA NUNCA ABAIXE A CABEÇA VIVA FELIZ A VIDA É ASSIM LEVANTA E SIGA EM FRENTE MAIS UM ELO DA CORRENTE QUE NÃO SE QUEBRARÁ VAMOS CELEBRAR

Chorus.
Muda ni sasa
muda ni sasa
muda ni sasa

Comments