Kitu gani by Natasha Shyrose
Play: Kitu Gani
https://soundcloud.com/natashashyrose/kitu-gani
Lyrics:
Unajifanya mjanja
Wakati unacheza moto na kiganja
Ulileta papara
Ukaniacha na maswali kichwani kama mia
Kama urembo ningejivunia
Kama ni raha ninakupatia
Kitu gani sijakifikia
Afanyacho mwenzangu
Chorus:
Kitu gani alicho nacho
Nisicho nacho
Jambo gani afanyalo
Nishindwalo mie
Unahaha haha
Mbona roho yako iko kwenye mashaka
Huwezi nisahau
Popote uendapo roho yako iko kwangu
Kama huyo ndiye unayemtaka
Nini kwangu unachofata
Na kile unachotaka
Ni udhaifu wa nafsi yako
Chorus:
Kitu gani alicho nacho
Nisicho nacho
Jambo gani afanyalo
Nishindwalo mie
Bridge:
Haipiti siku bila kukosa kukuwaza
Yale yote tuliyotenda wala sijutii
Hebu sema ukweli
Kwanini wajitapeli
Huwezi kujikeli
Kwa yaliyo ya kweli
Kusema ukweli kwanini wajitesa
Danganya vyote lakini roho yako yakucheka
Na kile unachotaka hapa utapata
Chorus:
Kitu gani alicho nacho
Nisicho nacho
Jambo gani afanyalo
Nishindwalo mie
Artist: Natasha Shyrose
Producer: Waterfly Studio
Executive Producer: Natasha Shyrose
Release: 26.08.2016
Comments
Post a Comment