MBALAMWEZI by NATASHA SHYROSE

 Mbalamwezi:
 
Verse1:
Mapenzi ni kitendawili, Yanapozidi wawili, Nimempa tuu mwili, Roho yangu iko kwako, Na wewe uko na mwengine, Ambaye akupendaye weye, Itabidi tuu nimpende, niliyenaye anipendae miye,Hebu nikuulize kitu longa longa longa, Ije itokee siku longa, longa, longa, Ikawa mimi na wewe tuu, Kitu gani hautotenda


Chorus: Ulitakiwa kuwa na miye, Nilitakiwa kuwa na weye, Ulitakiwa kuwa na miye Nakupenda penda nakutaka we, Nakupenda penda nakutaka we


Verse 2: Mbalamwezi inawaka, Moyo unataka inachotaka, Mapenzi kweli ni kidonda, Yanavyouma yanachonyota, Umeniacha nina tapatapa, Unanifanya nini weye kijana, Najua hata wewe unanitaka, Sijielewi nimedata, Hebu nikuulize kitu longa longa longa, Ije itokee siku longa, longa, longa, Ikawa mimi na wewe tuu, Kitu gani hautotenda


Chorus: Ulitakiwa kuwa na miye, Nilitakiwa kuwa na weye, Ulitakiwa kuwa na miye Nakupenda penda nakutaka we, Nakupenda penda nakutaka we, Mpenzi uwe wangu


Bridge: Moyo hebu kubali kupendwa, Acha kusononeka mbona wanitenda, Nitakuja kosa kote kote kwa sababu yako, Mimi na wewe ni damu damu, Malikia wa kutimiza zako hamu, Wewe uko huko akili zako ziko huku, Mimi niko huku akili zangu ziko huko


Chorus: Ulitakiwa kuwa na miye, Nilitakiwa kuwa na weye, Ulitakiwa kuwa na miye Nakupenda penda nakutaka we, Nakupenda penda nakutaka we. Mpenzi uwe wangu


Mpende akupendae, Kwani unayempenda Anapendwa na mwengine ,Ambae naye anapendwa kwengine ,Na yule ampendaye anampenda mwengine, Mapenzi kweli ni kitendawili, Kiza na mwangaza ,Kama mbalamwezi Kama mbalamwezi

Comments